1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChad

Kampeni za kura ya maoni itakayofanyika Desemba zaanza Chad

25 Novemba 2023

Taifa la Chad limeanza hii leo kampeni za kura ya maoni kuhusu katiba mpya inayotarajiwa kufanyika mwezi Desemba mwaka huu.

https://p.dw.com/p/4ZRfT
Tschad Junta Mahamat Idriss Deby Itno
Rais wa mpito wa Chad Jenerali Mahamat Idriss Deby ItnoPicha: Denis Sassou Gueipeur/AFP

Zoezi hilo litakuwa kipimo cha uhalali wa serikali ya kijeshi na utawala wa kiimla wa familila ya Deby Itno uliodumu kwa miaka 30.

Zaidi ya watu milioni 8.3 katika nchi hiyo kubwa lakini maskini ya ukanda wa Sahel, wanatazamiwa kushiriki kura ya maoni iliyopangwa kufanyika Desemba 17, ikiwa pia ni hatua muhimu kuelekea uchaguzi mkuu na kurejesha utawala wa kiraia.

Rais wa mpito wa Chad Jenerali Mahamat Idriss Deby Itno, ambaye uongozi wake wa kijeshi umetawala tangu mwaka 2021, aliahidi kukabidhi madaraka kwa raia na kufanya uchaguzi mwaka huu kabla ya kuuahirisha hadi mwaka 2024.