1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Israel yamuua kamanda mwandamizi wa Hezbollah

8 Januari 2024

Israel leo imefanya shambulizi la anga kusini mwa Lebanon na kumuua kamanda wa ngazi ya juu wa kundi la wanamgambo wa Hezbollah, kisa kinachozidisha wasiwasi wa kutanuka kwa mzozo unaolikumba eneo la Mashariki ya Kati.

https://p.dw.com/p/4azUJ
Shambulio la anga la Israel katika eneo la Naquora, Lebanon
Shambulio la anga la Israel katika eneo la Naquora, LebanonPicha: Ali Hashisho/XInhua/picture alliance

Duru kutoka ndani ya kundi la Hezbollah zinasema shambulio hilo liliilenga gari iliyokuwa ikiiendeshwa na Wissam al-Tawil ambaye ni kamanda wa kikosi cha siri cha Hezbollah kinafanya operesheni zake kwenye mpaka kati ya Israel na Lebanon.

Soma pia:  Wizara ya Afya Gaza yasema mashambulizi ya Israel yamewauwa watu 73

Shambulio hilo limetokea katika wakati mawaziri wa mambo ya kigeni wa Marekani na Ujerumani wanafanya ziara kwenye kanda hiyo kwa dhima ya kutuliza hamkani inayoweza kuigeuza vita kati ya Israel na kundi la Hamas kuwa mzozo wa kanda nzima.

Kwenye Ukanda wa Gaza kwenyewe vikosi vya Israel vimeendelea kufanya hujuma nzito vikililenga eneo la kati na kusini wa ukanda huo huku viongozi mjini Tel Aviv wakiapa kwamba kampeni yake ya kijeshi itadumu kwa miezi kadhaa inayokuja.