1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden na Xi kujadili mahusiano mema ya nchi zao

Bruce Amani
15 Novemba 2023

Rais wa Marekani Joe Biden na mwenzake wa China Xi Jinping, wako katika mji wa San Francisco, kuelekea mkutano unaosubiriwa kwa hamu kati ya viongozi hao wa mataifa mawili makubwa kiuchumi duniani.

https://p.dw.com/p/4Yp8x
Indonesien G20 Joe Biden und Xi Jinping
Picha: Saul Loeb/AFP/Getty Images

Biden na Xi watafanya mazungumzo pembezoni mwa mkutano wa kilele wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa nchi za Asia na Pasifiki - APEC jimboni California. 

Marais hao wanakutana wakati kukiwa na ongezeko la mivutano ya kibiashara, vikwazo na suala la Taiwan.

Xi na Biden wawasili San Francisco kwa mazungumzo muhimu

Kuelekea mazungumzo hayo, Biden amesema Marekani haitafuti kujitenga na China bali inataka kuimarisha mahusiano ya nchi hizo mbili yaliyozorota katika miaka ya hivi karibuni.

Mkutano wa kilele wa APEC unahudhuriwa na mataifa yapatayo 21 ambayo kwa pamoja yanachangia takriban asilimia 60 ya uchumi wa dunia.