1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUhispania

Barcelona wakosa nafasi ya kufungua mwanya wa pointi 10

27 Februari 2023

Barcelona walikosa nafasi nzuri kabisa ya kufungua uongozi wa pointi kumi dhidi ya mahasimu wao Real Madrid katika Ligi Kuu ya Uhispania La Liga hapo Jumapili.

https://p.dw.com/p/4O1v7
Spanien Xavi neuer Trainer von Barcelona
Picha: Gerard Franco/ZUMA Wire/imago images

Barca walikuwa ugenini wakicheza na Almeria na wakapoteza mechi hiyo moja bila kupitia kwa goli lililofungwa na El Bilal Toure kwenye dakika ya 24. Ilikuwa nafasi nzuri ya Barcelona kuushikilia usukani wa La Liga wakiwa na imani kubwa ya kushinda ubingwa huo mwishoni mwa msimu, baada ya Real Madrid kuzuiwa sare na Atletico katika dabi ya Madrid mnamo Jumamosi.

Hii ilikuwa mechi ya pili Barcelona kupoteza katika kipindi cha siku tatu baada ya kuondolewa na Manchester United katika mashindano ya Europa League katikati ya wiki iliyopita.

Kocha Xavi Hernandez wa Barca alikua na haya ya kusema.

"Tumeshindwa na nawapa pole mashabiki. Kwa mara nyengine leo ilikuwa siku muhimu na Real Madrid hawakushinda jana na tulistahili kuitumia nafasi hiyo na tukashindwa. Ili kushinda ligi tunahitaji kuwa na motisha zaidi kwa kuwa ni miaka mitatu sasa tangu tuishinde ligi," alisema Xavi.